Friday, 12 February 2010

day 5

mafunzo ya siku tano ya uandishi kwa kutumia mtandao ni ya kuvutia kwani yanaweza kunifunza mengi ambayo nilikuwa nahisi kama kitabu cha kusadikika kwani sijaweza kuamini kuwa name naweza kufikia hatua kama hii nilioipata katika mafunzo hayo. la kufurahisha ni kwamba nimeweza kujua jinsi ya kutengeneza blog, kuongeza art, kuedit, kuingiza picha na hata link ya mtu mwengine wakati kwa kutengeza blog. Mafunzo kama haya yawe endelevu ili kuweza kupata mafanikio zaidi. KUTOKANA NA MAFUNZO HAYO NITAENDELEZA BLOG YANGU ILI KUWEZA KUFIKIA MBALI ZAIDI NA KUPATA ZAIDI ELIMU LICHA YA KUWA NIPO KWANZA WA PILI WA MASOMO

France

mrembo

mtoto wa watu mzuri

Thursday, 11 February 2010

Abdulrazak Gurnah

Abdulrazak Gurnah ni mtunzi wa vitabu amezaliwa mwaka 1948 katika kisiwa cha Unguja. Mjumuiko wa Unguja ya Pemba ni Zanzibar eneo ambalo lipo katika eneo Afirka Mashariki. Alikwenda kusoma Britain katika mwaka 1968 na sasa ni amesomesha literature katika chuo kikuu cha Kent nchini huko. Pia ni msaidizi mhariri wa jarida la Wasafiri.

vitabu vya vitatu vya mwanzo ni pamoja na Memory of Departure (cha mwaka 1987), Pilgrims Way (cha mwaka 1988) na Dottie (cha mwaka 1990), vitabu vyengine ni pamoja na Paradise (1994).

Abdulrazak Gurnah sasa anaishi Brighton, East Sussex. alishawahi kupata tunzo ya uandishi kutoka Commonwealth.

tamasha hiloooooooooooo

Tamasha la www.busaramusic.org limeanzishwa mwaka 2003 likiwa na lengo la kuinua muziki wa Kiafrika hasa wa eneola Afrika mashariki. mwanzilishi wa tamasha hilo alikuwa ni Dj Yussuf aliyekuwa wazo la kuwasaidia wasanii wa kiafrika hasa wa eneno la Afrika shariki. Kwa mara ya saba sasa Zanzibar inashuhudia tena tamasha la Sauti za Busara kuanzia leo February 11 hadi February 16.tamasha hilo halitakuwa na kiingilio cha aina yoyote. Tamasha hilo litafanyika katika maeneo ya Ngome Kongwe likiwa na lengo la kukuza muziki wa kiafrika hasa wa Afrika mashariki. Kwa siku ya kwanza ya tamasha hilo kutakuwa na mzunguko wa utambulisho wa kuanza kwa tamasha hilo la Sauti za Busara kuanzia Viwanja vya kufurahishia watoto Kariakoo kupitia Radio Zanzibar, soko kuu la Darajani, Malindi Polisi Bandarini , Beit al Ajaib na kuishia Ngome kongwe. Miongoni mwa muziki utakaotumbuiza tamasha hilo ni pamoja na Taarabu asilia, dansi, bongo fleva na zenj fm. Katika tamsha hilo wasanii mbali mbali wa ndani na nje ya nchi watakotumbuiza tamasha akiwemo msanii Fresh Jumbe wa Tanzania ambae anafanyashughuli zake za muziki kwa hivi sasa nchini Japan, Banana Zoro wa Tanzania, Debo band kutoka Ethiopia, Juliana Kanyomozi kutoka Uganda bila ya kuwasahau madj maarufu kisiwani hapa Dj Yussuf na Dj Eddy.

Wednesday, 10 February 2010

Wangari Maathai

Wangari Muta Maathai amezaliwa April 1, 1940 katika kijiji cha Ihithe divisheni ya Tetu wilaya ya Nyeri nchini Kenya). Mkenya mwanaharakati wa mazingira na mwanasiasa. Amepata elimu yake nchini Marekani katika chuo cha Mtakatifu Scholastica na chuo kikuu cha Pittsburgh, pia chuo kuuu cha Nairobi nchini Kenya. Mnamo miaka ya 1970, Maathai alianzisha harakati the Green Belt Movement, taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayohusiana na masuala ya mazingira ikiwa na lengo la kupanda miti ili kuweza kuhifadhi mazingira pamoja na kutetea haki za wanawake. Mwaka 2004 alikuwa mwanamke wa kwanza wa Afrika na mwanamazingira na alipata tunzo ya Nobel Peace Prize kwa mchango wake wa kuwa na maendeleo endelevu, demokrasia na amani. Maathai alichaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Kenya na naibu waziri wa mazingira na maliasili katika serikali ya rais Mwai Kibaki baina ya January 2003 na November 2005. Yeye ni kutoka katika kabila la Wakikuyu.

Maisha yake na elimu yake.

Maathai amezaliwa April 1, 1940 katika kijiji cha Ihithe wilaya ya Nyeri maeneo ya kati ya milima ambayo yalikuwa yanatawaliwa na Wazungu wa Kenya. Familia yake ilikuwa ni la kabila la Wakikuyu, kabila maarufu nchini Kenya, na aliishi katika maeneo tofauti wakati akiwa mtoto. Katika mwaka 1943, familia ya Maathai waliishi eneo lililomilikiwa na wazungu la Rift Valley, karibu na mji wa Nakuru, mahali ambapo baba yake alikwenda kutafuta kazi. mwishoni mwa mwaka 1947 alirudi tena Ihithe na mama yake pamoja na kaka zake wawili kwa ajili ya kuanza elimu ya msingi kijijini na hakukuwa na shule eneo ambalo baba yake alikuwa akifanyia kazi. Baba yake alibakia kazini n alipofikia umri wa miaka minane aliungana na kaka zake katika shule ya msingi ya Ihithe.

Tuesday, 9 February 2010

mafunzo ya mtandao

Mafunzo ya jana yalikuwa ni mazuri kwani yameweza kutoka mwanga mkubwa kwangu ikizingatiwa kuwa ni yaanayoendena na wakati. Mafunzo hayo yamepanua uelewa wangu kwani kimeweza kujifunza zaidi kuhusiana na matumizi ya mtandao ikizingatiwa kuwa ni yanayoendana na wakati. Kulingana na mafunzo hayo naweza kupata zaidi faida ya matumizi ya mtandao na imeweza kunijulisha vyanzo zaidi vya habari vya ndani na nje. Kwa mfano mafunzo haya yametoa mwanga kwangu kwa kuweza kujua kwa jinsi gain unaweza kutumia mtandao ili kuweza kupata habari zaidi kuhusiana na jambo Fulani kupitia mtandao wa taasisi husika kama za bunge, serikali kuu na hata majarida tofauti yanayochapishwa ndani na nje ya nchi kupitia njia za mawasiliano ndani ya mtandao. Kulinganisha ukubwa wa masomo hayo naamini nikimaliza kipindi hiki itasaidia sana kupata mabadikiliko katika utendaji wangu wa kazi za kila siku. Mwalimu wa mafunzo hayo Peik Johansson ameshauri waandishi wa habari kutumia zaidi mtandao ili kuweza kupataa taarifa zinzoenda na wakati pamoja na kujiendeleza kielimu kwani mtando ni nji moja wapo ambayo inawatoa fursa za aina nyingi.
Piek Johansson amesema ili kuweza kufanikisha mafunzo hayo ni vyema kukubali kuyafanyia kazi kila siku kwa lengo la kujua matokeo ya dunia ya kila siku. Nao washiriki wa mafunzo hayo waneelezea vikwaoz vinavyowakabili kwa kushindwa kutumia mtandao ni pamoja na gharama za kulipia mtandao, hali ngumu za maisha pamoja na umbali wa maeneo yenye mtandao iwapo hawatakuwepo maeneo ya kazi.