Wednesday, 10 February 2010

Wangari Maathai

Wangari Muta Maathai amezaliwa April 1, 1940 katika kijiji cha Ihithe divisheni ya Tetu wilaya ya Nyeri nchini Kenya). Mkenya mwanaharakati wa mazingira na mwanasiasa. Amepata elimu yake nchini Marekani katika chuo cha Mtakatifu Scholastica na chuo kikuu cha Pittsburgh, pia chuo kuuu cha Nairobi nchini Kenya. Mnamo miaka ya 1970, Maathai alianzisha harakati the Green Belt Movement, taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayohusiana na masuala ya mazingira ikiwa na lengo la kupanda miti ili kuweza kuhifadhi mazingira pamoja na kutetea haki za wanawake. Mwaka 2004 alikuwa mwanamke wa kwanza wa Afrika na mwanamazingira na alipata tunzo ya Nobel Peace Prize kwa mchango wake wa kuwa na maendeleo endelevu, demokrasia na amani. Maathai alichaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Kenya na naibu waziri wa mazingira na maliasili katika serikali ya rais Mwai Kibaki baina ya January 2003 na November 2005. Yeye ni kutoka katika kabila la Wakikuyu.

Maisha yake na elimu yake.

Maathai amezaliwa April 1, 1940 katika kijiji cha Ihithe wilaya ya Nyeri maeneo ya kati ya milima ambayo yalikuwa yanatawaliwa na Wazungu wa Kenya. Familia yake ilikuwa ni la kabila la Wakikuyu, kabila maarufu nchini Kenya, na aliishi katika maeneo tofauti wakati akiwa mtoto. Katika mwaka 1943, familia ya Maathai waliishi eneo lililomilikiwa na wazungu la Rift Valley, karibu na mji wa Nakuru, mahali ambapo baba yake alikwenda kutafuta kazi. mwishoni mwa mwaka 1947 alirudi tena Ihithe na mama yake pamoja na kaka zake wawili kwa ajili ya kuanza elimu ya msingi kijijini na hakukuwa na shule eneo ambalo baba yake alikuwa akifanyia kazi. Baba yake alibakia kazini n alipofikia umri wa miaka minane aliungana na kaka zake katika shule ya msingi ya Ihithe.

No comments:

Post a Comment